Kikundi cha utamaduni kilianzishwa mwaka 1977, wakati wasanii walipokwenda
kushirikiana na wakulima na wafundi wa utamaduni sehemu ya Usukuma, Tanzania, Afrika
mashariki.
Tangia hapo kikundi hiki kiliendelea kueleweka kiutamaduni wa kiafrika
hasa wa kisukuma hapa nchii Denimaka. Sana sana kwa ajili ya michezo na ngoma, nyimbo na
mila ya jadi tuliendelea kuwaelewesha mambo hayo kwa wenzetu wadenish. Ushirikiano
ulingiza idara mbalimbali na miaka hizi tunayo matawi mengi ya kuwafahamisha
ifuatavyo.
Utamaduni Dance Troupe
Kikundi hiki cha ngoma unaelewesha vitendo ili waangaliaji waelewe maisha
ya waafrika, yasiyo ya vita na njaa peke yake, ila pia ni siku za kazi kawaida na siku za
kusherehekea pamoja. Vikundi vinaonyesha vitendo vya kuigiza ngoma za
kitanzania, pamoja
na nyimbo na sauti nyingi kama kuwina na mziki. Vile vile hadithi na maelezo kuhusu maisha
ya wasukuma wanaokaa karibu na ziwa Victoria, Nyanza huko kaskazini na magharibi mwa
Tanzania.
Wachezaji 6-12 waafrika na wadenish tunaigiza utamaduni na wakulima
wasukuma kwa njia ya kuonyesha na kutumia vifaa, vyombo na mawaazi na mapambo kutoka huko
Afrika. Pia tunawakaribisha waangaliaji kuingia kucheza kipindi fulani pamoja na
kikundi.
Mara fulani tunapenda kufika walimu wanne kufundisha vitendo, nyimbo na
ngoma kwa watoto au vijana wanaopenda kufahamu na wasiyo ogopa kutoa jasho kutumia mwili
kwa nguvu pamoja na sauti.
Kutokana na kazi ya kuonyesha na kufundisha utamaduni wa kiafrika, mambo hayo hueneza sana
nchii Denimaka nzima, na miaka hii unaweza kuona vikundi 20+, wachezaji wanaopenda ngoma
za kiafrika sehemu mbali mbali hapa Denimaka, Swedeni na Norway.
Utamaduni Summercamp
Mwaka 1983 tulianza kupanga mara ya kwanza workshop vya vikundi
vyote.
Utamaduni summercamp ya '83 tulipanga weekend nzima kukutana watu 50 katika sehemu ya
msitu, Djursland, Denimaka.
Tangia hapo sifa ya Utamaduni Summercamp ilienea kweli na siku hizi tuko
watu mia nne tunapofika msituniwiki nzima kucheza na vifaa vyetu vya kiafrika na vya
kidenish na kulala kwenye mahema na kupika vyakula na kula kwa pamoja kiujamaa.
Kucheza
Kila mwaka, wakati wa baridi wa kukaa ndani ya nyumba, mwezi wa pili kuna
kikundi kimoja kinajiita "Watoto na wengine" wanaokaa kisiwani Fyn, kusini mwa
Denimaka wanatukaribisha "Vinter-kucheza" weekend nzima. Hapo kwenye shule kubwa
tunacheza na tunaongea, watoto na wazima na vijana, kwa ajili ya kugawana upendo wa
kucheza ngoma.
Utamaduni
Emmelev kaervej 1
8500 Grenaa
Denmark, Europe
info@utamaduni.dk
Tembelea
Mtandao wa Taifa Tanzania
Soma "UMOJA WA MATAIFA OFISI YA
IDARA YA HABARI TAARIFA YA ULIMWENGU JUU YA HAKI ZA BINADAMU UTANGULIZI"
|